Roland Benito, ambaye anakifanyia kazi Kitengo Huru cha Malalamiko kuhusu Polisi, ametumwa pamoja na mfanya kazi mwenza kwenda kuwahoji maafisa wawili wa polisi ambao wameitika mwito wa hali ya dharura. Mlinzi mmoja wa jela amejirusha kutoka kwa dirisha ya chumba chake kilicho katika orofa ya nne, punde tu maafisa hawa wawili wanapowasili baada ya kupata malalamishi kuhusu muziki wa sauti ya juu kutoka kwa chumba hicho. Kwa mtazamo wa juu, hakuonekani kuwa na jambo lolote la kukisiwa kuhusu hali hii ila pale inapotambulika kuwa mlinzi huyu wa jela ni baba ya rafiki wa dhati wa mjukuu wake Roland wanaosoma pamoja, Roland anasikia kuwa mfungwa mmoja amefariki kwenye jela pale alipokuwa akifanya kazi na kuwa mlinzi huyu wa jela amekuwa akihisi kutishiwa na anayefuatwa. Je, inawezekana kuwa haya hayakuwa mauaji ya binafsi hatimaye? Anne Larsen, mwandishi wa habari kutoka TV2 East Jutland, pia ananukuu hadithi ya vifo hivi. Wakati wa utafiti wake, anatambua kifo kingine, wakili wa utetezi aliyefariki katika ajali ya barabarani. Anatambua kuwa vifo hivi vyote vinahusishwa na mfungwa mmoja, Patrick Asp muuaji wa mtoto, ambaye alihukumiwa kifungo cha maisha baada ya kumuua mtoto wake mdogo wa kike, na ambaye ni mfungwa katika jela ambayo mlinzi yule wa jela alikuwa akifanya kazi.
The Cleaner ni mchezo wa kuigiza wa kihalifu wenye matukio sita.
Inger Gammelgaard Madsen (b. 1960) ni mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Inger Gammelgaard Madsen ana uasilia wa kisomo cha uchoraji wa vielelezo. Alianza kuandika hadithi zinazohusu uhalifu “Dukkebarnet” katika mwaka wa 2008. baada ya kitabu hiki, ameandika vitabu vingine kadhaa vinavyohusu uhalifu. Baadhi ya vitabu hivi ni «Drab efter begæring” (2009), “Slangers gift” (2014), «Dommer og bøddel” (2015) na “Blodregn” (2016).